TALAKA KATIKA UISLAMU.

Leo ndugu zangu ningependa tujifunze mambo mambo kadhaa kuhusu talaka, kwasababu talaka ipo na haikwepeki katika mfumo wa maisha yetu ya kila siku. tujifunze mada hii kwa njia ya maswali yafuatayo;
              1.kuna aina ngapi za talaka katika uislamu?

               2.Talaka tatu hutolewa wakati gani? na kwa kosa gani?

              3.mume alie muacha mkewe kwa talaka tatu anaweza kumrejea?

              4.ni mambo gani haramu kwa mume alie muacha mkewe kwa talaka tatu kutendewa au mtalaka wake?

            5.neno talaka rejea lina maana gani katika uislamu?

            6.nini haki za mke alie achwa toka katika mali za mume aliye mwacha?
Hayo ni baadhi ya maswali yahusuyo talaka ambayo kila mmoja anawajibu wa kufahamu majibu yake ili tuweze isaidia jamii yetu pindi inapo tokea suala la talaka.

1.  Kwanza tukianza na swali la kwanza ni kwamba kwanza yatupasa kufahamu maana ya talaka kwa kuwa ndio msingi wa mada hii.
Talaka ni kufungua fungo la ndoa kwa tamko bayana au kwa kinaya (isiyo moja kwa moja ). na vigawanyo vya talaka ni kama vifuatavyo:
*talaka ya sunnah hii ni ile ambayo mume humuacha mkewe katika utwahara ambao hajawahi kukutana naye kimwili.
*Talaka ya bid'ah hii ni ile ambayo mume humuacha mkewe akiwa katika siku zake za ada, au katika kipindi cha damu ya uzazi au katika twahara aliomuingilia au kumuacha talaka tatu kwa mpigo mmoja. mwenye kutoa talaka ya aina hii huwa anapata madhambi lakini talaka yenyewe hua  imepita ( imesihi/kukubalika) ila ile ya tatu huhesabiwa kuwa ni moja tu.
*talaka baain ni ile ambayo mume anamuacha mkewe akakosa haki ya kumrejea  kwa kuwa eda imekwisha. hivyo, mume huyo akawa ni mposaji kama waposaji wengine na mke akikubali inabidi mume apose, atoe mahari na ifungwe ndoa upya.
*Talaka rejea ni ile ambayo mume anamiliki haki ya kumrejea mtalaka wake, huku ni mume kumrejea mkewe katika kipindi cha eda ya kuachwa talaka ya kwanza au ya pili.

baada ya ufafanuzi huo, tuje katika msingi wa swali lenyewe, ni kwamba zipo aina tofauti za kutoa talaka , nazo ni kama zifuatazo;
a) talaka ya bayana: hii ni talaka ilio wazi kabisa isiyo na utata wa aina yoyote, nayo ni kama kusema "nimekuacha " na tamko hili si lazima ukusudie kwani tamko lako linatosha.
b)talaka kinaya (isiyo ya bayana ) hii ni lazima ukusudie talaka kwa tamko lako si bayana , kama kusema " nenda kwa ndugu zako " au " usiseme na mimi " na yanayo fanana na hayo. ikiwa talaka imenuiwa basi itakuwa imetumika.
c)talaka ya hapo kwa hapo ni ile ambayo pindi inapo tolewa mke huachika papo hapo bila ya kuchelewa, hiyo ni kusema " wewe umeachika "  baada ya mume kutamka hayo mkewe atakuwa ameachika.
d)talaka ya kutungika: ni ambayo mume ameitungika juu ya kitu kingine kuwa kitu hicho akikifanya au akikiacha atakua ameachika. mfano ni mume kusema " ukitoka hapa nyumbani bila ya ruhusa yangu utakua umeachika " na yanayo fanana na hayo.
e)talaka ya khiyari : hii ni mume kumwambia mkewe nimekupatia khiyari kutengana na mimi au kuachana na mimi. Akichagua kutengana talaka itakuwa imesihi/ imekubalika. ushahidi wa talaka hii upo katika Quran sura ya 33 ( surat ahzaab ) aya ya 28.
f)talaka kwa uwakala au maandishi: mume kama atamuwakilisha mtu mwingine kumuacha mkewe au akamuandikia mkewe talaka akimuarifu katika maandishi hayo kuwa amemuacha, mke atakuwa ameachika.
g)talaka kwa kuharamisha: hii ni kusema kwa mume kumwambia mkewe wewe ni haramu kwangu au unakuwa haramu, kama atakusudia kwa tamko hilo talaka, itakua talaka. Na kama atakusudia mzaha itakuwa mzaha lakini atawajibika mume huyo kwa tamko hilo kafara ya mzaha wake.

2. Ama kuhusu swali la pili ni kuwa hakuna wakati wowote ambapo mume anakubaliwa kisheria kutoa talaka tatu kwa mara moja au kikao kimoja. kufanya hivyo ni kosa na inahesabiwa kuwa ni talaka moja peke yake katika sheria ya kiislamu.

3. Ama katika swali la tatu ni kuwa ikiwa mume amemuacha mkewe talaka tatu mara moja, huhesabiwa ni moja tu. Ikiwa kwa hilo kwa hilo unamaanisha kumuacha mkeo kwa kumpatia talaka ya kwanza, kisha ya pili, mpaka ikafika ya tatu, basi haiwezekani kwa hao wawili kurudiana kama mume na mke mpaka kwanza mke aolewe na mume mwingine  wakutane kimwili kisha aachwe. hapo ndio itawezekana kumrudia tena kwa kufuata utaratibu wote wa ndoa. ushahidi upo ktk qurani ( sura ya 2 : 230 ).

4. Ama kuhusu swali la nne ni kuwa haifai kwa watalaka kudhulumiana kwa njia moja au nyingine. pia haifai kwao kuweka chuki na uadui baina yao na kutoa siri walizo weka baina yao kwa wengine. kuoana ni kwa wema na ikitokea sababu ya kuachana basi tuachane kwa wema. pia haifai kwa mume kuchukua kutoka kwa mtalaka wake alivyo mpa kama hadiya kwa njia yoyote ile na vile vile si halali kwa mke kuchukuwa visivyo vyake kwa njia yoyote ile.

5.Ama kuhusu neno talaka rejea ni kama tulivyo  lielezea hapo juu kuwa kuwa hii ni ile talaka ambayo mume anamiliki haki ya kumrejea mtalaka wake nako ni kumrejea  mkewe katika kipindi cha eda ya kuachwa talaka ya kwanza au ya pili. ushahidi Quran ( sura 2 : 228).

6.Ama katika swali la mwisho ni kuwa pindi mke anapo achwa na mume anawajibu wa kumtazama kwa makazi, chakula, mavazi, matibabu, na yote anayo fanyiwa mke akiwa katika ndoa. Ama katika mali mke hatakuwa na haki yoyote isipokuwa kama walikuwa na ushirika katika hilo. ikiwa hali ni hiyo kila mmoja atapata haki yake kama walivyo patana wao katika unyumba wao na ile kazi inavyo kwenda, mke atakuwa na yale mali aliyo patiwa na mtalaka wake wakiwa katika ndoa. haifai kwa mume kuchukua alivyompa kwa njia yoyote ile. ushahidi Qurani ( sura 2 : 229 ) na pia katika Qurani ( sura 4 : 20 ).

Naamini tumejifunza machache katika mengi yahusuyo talaka.
author: yurys law
number: +255656558788
email: ulimwengujuma2014@gmail.com

 رَبِّ اجْعَلْ هَـَذَا بَلَدًا آمِنًا وَارْزُق ْأَهْلَهُ مِنَ الثَّمَرَاتِ مَنْ آمَنَ مِنْهُم بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ     (البقرة:126)
Ee Mola wangu! Ufanye huu uwe mji wa amani, na uwaruzuku watu wake matunda, wale wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho. (Al-Baqarah: 126)
رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ      
رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ (البقرة 127- 128)
Ewe Mola wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi.
Ewe Mola wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe ummah uliosilimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. (Al-Baqarah: 127-128)).

رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ (البقرة 201  )  
Mola wetu, tupe duniani mema, na Aakhirah mema, na utulinde na adhabu ya Moto. (Al-Baqara 201)

رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ (البقرة 250 )
Mola wetu! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri (Al-Baqarah: 250)

رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلاَنَا فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ  (البقرة 286)
Mola wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Usitutwike tusiyoyaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. (Al-Baqarah: 286)

رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ  (آل عمران 8  )
Mola wetu! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwishatuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. (Al-'Imraan: 8)

رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ  (آل عمران 16)
Mola wetu! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu, na tuepushe na adhabu ya Moto.  (Al-Imran 16)

رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاء  (آل عمران 38]
Mola wangu! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unayesikia maombi. (Al-'Imraan: 38)

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلَتْ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ  (آل عمران 53)
Mola wetu! Tumeyaamini uliyoyateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (Al-'Imraan: 53)

ربَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَِ    (آل عمران 147)    
Mola wetu! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri (Al-'Imraan: 147)

رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَذا بَاطِلاً سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلإِيمَانِ أَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الأبْرَارِ رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلاَ تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّكَ لاَ تُخْلِفُ الْمِيعَاد ِ
(آل عمران 191-194)
Mola wetu! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika! Basi tukinge na adhabu ya Moto.
Mola wetu! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na waliodhulumu hawana wasaidizi.
Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu; nasi tukaamini. Basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema.
Mola wetu! Na utupe uliyotuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Qiyaamah. Hakika Wewe huvunji miadi. (Al-'Imraan :191-194)

 رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا  (النساء:75)
Mola wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anayetoka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. (An-Nisaa: 75)
رَبَّنَا آمَنَّا فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ   (المائدة:83)
Mola wetu! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia (Al-Maaidah:  83)

رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ    (الأعراف23) 
Mola wetu! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika  (Al-A'raaf: 23)

رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (الأعراف 47)   
Mola wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu waliodhulumu (Al-A'raaf: 47)

رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ   (الأعراف:89)
Ewe Mola wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanaohukumu.  (Al-A'raaf: 89)

رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ  ( الأعراف 126)
Ewe Mola wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. (Al-A'raaf: 126)

أَنتَ وَلِيُّنَا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الْغَافِرِينَ (الأعراف 155)         
Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria (Al-A'raaf: 155)

حَسْبِيَ اللّهُ لا إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ (التوبة  129) 
Allaah ananitosheleza. Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola wa 'Arsh tukufu. (At-Tawbah: 129)

رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ   (يونس85-86)
Ewe Mola wetu! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu.
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri  (Yuwnus: 85 – 86 )

رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ وَإِلاَّ تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ   (هود  74)
Ewe Mola wangu! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na ujuzi nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika waliopata khasara. (Huwd: 47)

رَبِّ اجْعَلْنِي مُقِيمَ الصَّلاَةِ وَمِن ذُرِّيَّتِي رَبَّنَا وَتَقَبَّلْ دُعَاء    (إبرهيم-40)
Mola wangu! Nijaalie niwe mwenye kusimamisha Swalaah, na katika dhuriya zangu pia. Ewe Mola wetu, na ipokee dua yangu. (Ibraahiym: 40)

رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَاب   (إبرهيم41 )  
Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu(Ibraahiym: 41)

أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنُيَا وَالآخِرَةِ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ  (يوسف:101)
Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema(Yuwsuf: 101)

رَّبِّ ارْحَمْهُمَا كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا (الإسراء 24)
Mola wangu! Warehemu kama walivyo nilea utotoni. (Al-Israa: 24)

 رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا   (الإسراء-80)  
Mola wangu! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie. (Al-Israa: 80)

رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا (الكهف10) 
Mola wetu! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu. (Al-Kahf: 10)

رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي  وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي  وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي يَفْقَهُوا قَوْلِي (طه 25-28)  
Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu. (Twaahaa: 25-28)

 رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا (طه 114)  
Mola wangu! Nizidishie ilimu. (Twaahaa: 114)

لا إِلَهَ إِلا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ (الأنبياء87) 
Hapana mabudiwa wa haki isipokuwa Wewe Subhaanaka Uliyetakasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. (Al-Anbiyaa: 87)

رَبِّ لاَ تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ   (الأنبياء 89 )  
Mola wangu! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi
(Al-Anbiyaa: 89)

رَبِّ أَنْزِلْنِي مُنْزَلاً مُبَارَكاً وَأَنْتَ خَيْرُ الْمُنْزِلِينَ (المؤمنون 29)
Mola wangu! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora wa wateremshaji (Al-Mu'minuwn 29)

رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ (المؤمنون97-98) 
Mola wangu! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani.  Na najikinga kwako, Mola wangu, wasinikaribie.(Muuminuwn: 97-98)

  رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (المؤمنون  109)  
Mola wetu! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu. (Muuminuwn: 109)

رَّبِّ اغْفِرْ وَارْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ (المؤمنون 118)
Mola wangu! Samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu
(Al-Muuminuwn: 118)

رَبِّ هَبْ لِي حُكْماً وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ   وَاجْعَلْ لِي لِسَانَ صِدْقٍ فِي الأَخِرِين 
 وَاجْعَلْنِي مِنْ وَرَثَةِ جَنَّةِ النَّعِيمِ  (الشعراء 83-85)
Mola wangu! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadayeNa unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. (Ash-Shu'araa: 83-85)
رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي (القصص 16)
Mola wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe (Al-Qaswas: 16)

رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِلْمُجْرِمِينَ (القصص 17)
Mola wangu! Kwa ulivyonineemesha, basi mimi sitokuwa kabisa msaidizi wa wakosefu (Al-Qaswas: 17)
رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ (القصص 21)
Mola wangu! Niokoe na watu madhaalimu(Al-Qaswas: 21)

رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَاماً الفرقان 65 )
Mola wetu! Tuondolee adhabu ya Jahannam. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi (Al-Furqan 65)

  رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَاماً (الفرقان 74)
Mola wetu! Tupe katika wake zetu na wetoto wetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachaji Allaah. (Al-Furqaan: 74)

رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحاً تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ (النمل 19)
Ee Mola wangu! Nizindue niishukuru neema yako uliyonineemesha mimi na wazazi wangu, na nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako wema. (An-Naml: 19)
وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ  (غافر 44)
Nami namkabidhi Allaah mambo yangu. Hakika Allaah Anawaona waja wake.(Ghaafir: 44)

رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَى وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَصْلِحْ لِي فِي ذُرِّيَّتِي إِنِّي تُبْتُ إِلَيْكَ وَإِنِّي مِنْالْمُسْلِمِينَ  (الأحقاف 15)
Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizo nineemesha mimi na wazazi wangu, na nitende mema unayo yapenda. Na unitengenezee dhuriya zangu. Hakika mimi nimetubu kwako, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. (Al-Ahqaaf: 15)

رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ  (الدخان 12)  
Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. (Ad-Dukhaan: 12)

 رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلاَ تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ  (الحشر 10)
Mola wetu! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu. (Al-Hashr: 10)
 رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ  
 رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ (الممتحنة 4-5)
Mola wetu! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.
Mola wetu! Usitufanyie mtihani kwa waliokufuru. Na tusamehe, Mola wetu. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima(Al-Mumtahina: 4 -5 )
 رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ  (التحريم 8)  
Mola wetu! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu .(At-Tahriym: 8)
 رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِيَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَلَا تَزِدِ الظَّالِمِينَ إِلَّا تَبَارًانوح:28)
Mola wangu! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliyeingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.

UTARATIBU WA KUSALI SALA YA MAITI.


Ndugu zangu miongoni mwa vitu ambavyo waislamu wengi wana vipuuza ni mambo yote yanayo muhusu maiti kama vile kuosha maiti, kushona sanda pamoja na kumkafini(kumvika sanda), na kumsalia maiti, mambo hayo waislamu tunayapuuza na kudhani kwamba ni mambo yanayo takiwa kufanywa na mashekhe basi. yaani inafikia hatua mtu anafiwa na mwanae ati anatafuta shekhe wa kuja kumuosha, kumvika sanda pamoja na kumsalia maiti wake, ndugu zangu hii ni aibu kubwa kwasababu mambo hayo ni wajibu kila muislamu aweze kuyatambua.

leo nitaeleza kuhusu sala ya maiti na mungu akipenda siku nyingine tutaelekezana kuhusu mambo mengine yalio baki yanayo muhusu maiti. ndugu zangu sala ya maiti ina rakaa nne, sala hiyo huswaliwa bila ya rukuu wa sijda ni sala inayo saliwa wima kwa wima na safu yake yaani maamuma wanatakiwa wajipange mistari witiri kwa maana mistari inatakiwa iwe1, 3, 5, 7, 9 n.k  ni sunna kwa maamuma kujipanga namna hiyo.

Na sala hii ya maiti hua haina adhana wala haina iqama ni kusimama tu na kuita watu waje waungane katika sala hiyo kwa mwenye kuweza .

RAKAA YA KWANZA.
rakaa ya kwanza imamu ataleta takbiratul ihramu(allahu akbaru) na maamuma nao watasema hivyo hivyo kama alivyo sema imamu lakini si kwasauti maamuma wataisema ndani ya moyo(kimya kimya) alafu maamuma na imamu wote watasoma suratil faatiha(alhamdu....) kimya kimya bila ya kuongeza sura nyingine.

RAKAA YA PILI
Baada ya kusoma suuratil faatiha(alhamdu.....) imaamu atesema tena takbira (allahu akbaru) kwa sauti, kisha maamuma nao wataleta takbira hiyo moyoni(kimya kimya) kisha maamuma na imamu katika rakaa hii ya pili wote watamslia mtume s.a.w kwa moyoni si kwasauti(kimya kimya) ambayo ni allahuma swalli alaa muhammad wa alaa alii muhammad, kama swalayta alaa ibraahim, wa alaa alii ibraahim, wabaarik alaaa muhammad, waalaa alii muhammad, kamaa barakta alaaa ibraam waalaaaliii ibraahim, fil-aalamiin, innaka hamiidum-majiidu.

RAKAA YA TATU
Baada ya kumsalia mtume s.a.w, imamu ataleta tena takbira(allahu akbaru) kisha maamuma na imamu wote watamuombea dua maiti wao kwa kadri ya uwezo wako lakini si kwa kiswahili kwasababu lugha inayo tumika ndani ya sala ni kiarabu kwahiyo kama si mtaalamu saana wa lugha hiyo unaweza ukamuombea maiti huyo mungu amsamehe madhambi yake, kwaiyo katika rakaa ya tatu utaomuombea dua maiti huyu tunae msalia yoyote unayo ifahamu.

RAKAA YA NNE
Baada ya kumuombea maiti dua, imamu ataleta tena takbira(allahu akbar) kisha imamu na maamuma wote wata omba dua(kimya kimya) ya kuwaombea waislamu na waumini wote walioko hai na walio tangulia akhera, kwahiyo katika rakaa hii ya nne utaomba dua kwa waumini wote, na waislaamu wote na jamii nzima kwa ujumla, utasoma dua yoyote unayo ifahamu laikni kwa kiarabu.

kisha baada ya hapo imamu atatoa salaamu kama ya sala za kila siku tunazo sali majumbani na miskitini mwetu, atatoa salaamu kwa kuanzia kulia kwenda kushoto, kisha inafuata hatua nyingine ya kulichukua jeneza yaani kum-beba maiti wetu na kwenda nae kumsitiri mahala pake(kaburini mwake) inshaaallah hapo tutakua tumemaliza sala ya maiti kuanzia rakaa ya mwanzo mpaka ya mwisho.
hakuna mwanadamu alie kamilika.
coment neno lolote ambalo labda nimekosea katika mapungufu ya kibinadamu au nimesahau kipengele chochote katika mada hiyo au waweza kuandika neno lolote kutokana na ulivyo elewa mada hii.

TOFAUTI KATI YA BIBLIA NA QURANI.



                                       Image result for image of quranImage result for image of bible   
leo tujifunze kuhusu tofauti za kimsingi zinazo tofautisha baina ya qurani na biblia, zipo tofauti nyingi saana lakini tusome baadhi ya tofauti hizo ili tuweze kuongeza kitu akilini mwetu.
1. Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu visivyo pungua 73 kwa mujibu wa madhehebu ya wakatoliki na kuna(biblia) yenye mkusanyiko wa vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya waprotestant na kuna ile ya yenye vitabu 81 kwa madhehebu ya kanisa la kiethiopia. vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40, wakati Qurani ni kitabu kimoja kilichotoka kwa mwenyezi mungu mmoja na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.

2.Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno yamwenyezi mungu, mitume na maoni ya wanahistoria, wakati Qurani ni maneno ya mwenyezi mungu peke yake, hata maneno ya muhammadi hayamo katika qurani.

3. Injili ya mathayo, luka, marko na yohana zinaelezea historia ya yesu kama ilivyo simuliwa na na wafuasi wake, katika agano jipya na agano la kale yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya mitume mbali mbali. kumbu kumbu la torati (na sio torati yenyewe), siyo tu ni ujumbe wa mwenyezi mungu bali pia ni historia ya maisha ya nabii mussa. wakati qurani si historia ya muhammadi kama ilivyo simuliwa na maswahaba zake. qurani inataja habari za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

4. Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu mitume hao, ndio maana wanazuoni wa kikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika hayo lini.
kwa mfano katika biblia ilio tolewa na collins iitwayo Revised standard version ya mwaka 1971 ukurasa wa 12-17 imeandikwa kuwa mwandishi wa samweli hajulikani , pia hajulikani mwandishi wa 2samweli, 1wafalme, 2wafalme, 1mambo ya nykati, esta, yona, ayubu na habakuki.
Hali kadhalika mpaka leo kuna wasi wasi kama kitabu cha waebrania kiliandikwa na paulo au na mtu mwingine. Encyclopaedia Britanica inakiri kuwa mpaka hivi sasa hakuna uhakika jinsi gani au ni wapi vitabu vinne vya injili vilipatikana. wakai qurani yote iliandikwa wakati wa uhai wa muhammadi na kuhifadhiwa na mamia ya watu.

5.Injili nne zilizomo katika agano jipya siyo injili zote zilizo andikwa, zilikuwapo injili nyingine nyingi, ila kwa amri ya mfalme constantine ilifanyika sinodi ( mkutano wa wakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe.
Injili kadhaa zilikataliwa kama vile injili ya Barnabas, injili ya marcion, injili ya Basilides, injili ya maryam, injili ya yuda, injili ya philipo, injili ya wahebrania, injili ya nazareti, injili ya Bartholomew na nyingine nyingi.
Na katika historia ya kanisa viko vitabu vilivyo kubaliwa na baadae kukataliwa na kinyume chake. Ni binadamu walio kuja baadae ndio walio kuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la mungu na lipi lisiwe. wakati katika uislamu hakukua na Ijitimai yoyote ilio kaa kuamua sura ipi iwe qurani na ipi isiwe katika qurani.

hizo ni baadhi ya tofauti kati ya qurani na biblia ambazo wengi wetu hatukuzifahamu hapo kabla , naomba mniombee afya kwa mwenyezimungu ili niweze kuandika habari mbali mbali zenye manufaa katika jamii yetu.
wako mwandishi: ulimwengu khatwibu.
   ulimwengujuma2014@gmail.com
              +255684996890