leo tujifunze kuhusu tofauti za kimsingi zinazo tofautisha baina ya qurani na biblia, zipo tofauti nyingi saana lakini tusome baadhi ya tofauti hizo ili tuweze kuongeza kitu akilini mwetu.
1. Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu visivyo pungua 73 kwa mujibu wa madhehebu ya wakatoliki na kuna(biblia) yenye mkusanyiko wa vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya waprotestant na kuna ile ya yenye vitabu 81 kwa madhehebu ya kanisa la kiethiopia. vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40, wakati Qurani ni kitabu kimoja kilichotoka kwa mwenyezi mungu mmoja na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.
2.Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno yamwenyezi mungu, mitume na maoni ya wanahistoria, wakati Qurani ni maneno ya mwenyezi mungu peke yake, hata maneno ya muhammadi hayamo katika qurani.
3. Injili ya mathayo, luka, marko na yohana zinaelezea historia ya yesu kama ilivyo simuliwa na na wafuasi wake, katika agano jipya na agano la kale yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya mitume mbali mbali. kumbu kumbu la torati (na sio torati yenyewe), siyo tu ni ujumbe wa mwenyezi mungu bali pia ni historia ya maisha ya nabii mussa. wakati qurani si historia ya muhammadi kama ilivyo simuliwa na maswahaba zake. qurani inataja habari za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.
4. Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu mitume hao, ndio maana wanazuoni wa kikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika hayo lini.
kwa mfano katika biblia ilio tolewa na collins iitwayo Revised standard version ya mwaka 1971 ukurasa wa 12-17 imeandikwa kuwa mwandishi wa samweli hajulikani , pia hajulikani mwandishi wa 2samweli, 1wafalme, 2wafalme, 1mambo ya nykati, esta, yona, ayubu na habakuki.
Hali kadhalika mpaka leo kuna wasi wasi kama kitabu cha waebrania kiliandikwa na paulo au na mtu mwingine. Encyclopaedia Britanica inakiri kuwa mpaka hivi sasa hakuna uhakika jinsi gani au ni wapi vitabu vinne vya injili vilipatikana. wakai qurani yote iliandikwa wakati wa uhai wa muhammadi na kuhifadhiwa na mamia ya watu.
5.Injili nne zilizomo katika agano jipya siyo injili zote zilizo andikwa, zilikuwapo injili nyingine nyingi, ila kwa amri ya mfalme constantine ilifanyika sinodi ( mkutano wa wakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe.
Injili kadhaa zilikataliwa kama vile injili ya Barnabas, injili ya marcion, injili ya Basilides, injili ya maryam, injili ya yuda, injili ya philipo, injili ya wahebrania, injili ya nazareti, injili ya Bartholomew na nyingine nyingi.
Na katika historia ya kanisa viko vitabu vilivyo kubaliwa na baadae kukataliwa na kinyume chake. Ni binadamu walio kuja baadae ndio walio kuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la mungu na lipi lisiwe. wakati katika uislamu hakukua na Ijitimai yoyote ilio kaa kuamua sura ipi iwe qurani na ipi isiwe katika qurani.
hizo ni baadhi ya tofauti kati ya qurani na biblia ambazo wengi wetu hatukuzifahamu hapo kabla , naomba mniombee afya kwa mwenyezimungu ili niweze kuandika habari mbali mbali zenye manufaa katika jamii yetu.
wako mwandishi: ulimwengu khatwibu.
ulimwengujuma2014@gmail.com
+255684996890
Ushuhuda
ReplyDeleteNilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.
Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:
✅ Maneno ya mapenzi
✅ Tahadhari za Ujauzito
✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.
📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159
Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!