UTARATIBU WA KUSALI SALA YA MAITI.
Ndugu zangu miongoni mwa vitu ambavyo waislamu wengi wana vipuuza ni mambo yote yanayo muhusu maiti kama vile kuosha maiti, kushona sanda pamoja na kumkafini(kumvika sanda), na kumsalia maiti, mambo hayo waislamu tunayapuuza na kudhani kwamba ni mambo yanayo takiwa kufanywa na mashekhe basi. yaani inafikia hatua mtu anafiwa na mwanae ati anatafuta shekhe wa kuja kumuosha, kumvika sanda pamoja na kumsalia maiti wake, ndugu zangu hii ni aibu kubwa kwasababu mambo hayo ni wajibu kila muislamu aweze kuyatambua.
leo nitaeleza kuhusu sala ya maiti na mungu akipenda siku nyingine tutaelekezana kuhusu mambo mengine yalio baki yanayo muhusu maiti. ndugu zangu sala ya maiti ina rakaa nne, sala hiyo huswaliwa bila ya rukuu wa sijda ni sala inayo saliwa wima kwa wima na safu yake yaani maamuma wanatakiwa wajipange mistari witiri kwa maana mistari inatakiwa iwe1, 3, 5, 7, 9 n.k ni sunna kwa maamuma kujipanga namna hiyo.
Na sala hii ya maiti hua haina adhana wala haina iqama ni kusimama tu na kuita watu waje waungane katika sala hiyo kwa mwenye kuweza .
RAKAA YA KWANZA.
rakaa ya kwanza imamu ataleta takbiratul ihramu(allahu akbaru) na maamuma nao watasema hivyo hivyo kama alivyo sema imamu lakini si kwasauti maamuma wataisema ndani ya moyo(kimya kimya) alafu maamuma na imamu wote watasoma suratil faatiha(alhamdu....) kimya kimya bila ya kuongeza sura nyingine.
RAKAA YA PILI
Baada ya kusoma suuratil faatiha(alhamdu.....) imaamu atesema tena takbira (allahu akbaru) kwa sauti, kisha maamuma nao wataleta takbira hiyo moyoni(kimya kimya) kisha maamuma na imamu katika rakaa hii ya pili wote watamslia mtume s.a.w kwa moyoni si kwasauti(kimya kimya) ambayo ni allahuma swalli alaa muhammad wa alaa alii muhammad, kama swalayta alaa ibraahim, wa alaa alii ibraahim, wabaarik alaaa muhammad, waalaa alii muhammad, kamaa barakta alaaa ibraam waalaaaliii ibraahim, fil-aalamiin, innaka hamiidum-majiidu.
RAKAA YA TATU
Baada ya kumsalia mtume s.a.w, imamu ataleta tena takbira(allahu akbaru) kisha maamuma na imamu wote watamuombea dua maiti wao kwa kadri ya uwezo wako lakini si kwa kiswahili kwasababu lugha inayo tumika ndani ya sala ni kiarabu kwahiyo kama si mtaalamu saana wa lugha hiyo unaweza ukamuombea maiti huyo mungu amsamehe madhambi yake, kwaiyo katika rakaa ya tatu utaomuombea dua maiti huyu tunae msalia yoyote unayo ifahamu.
RAKAA YA NNE
Baada ya kumuombea maiti dua, imamu ataleta tena takbira(allahu akbar) kisha imamu na maamuma wote wata omba dua(kimya kimya) ya kuwaombea waislamu na waumini wote walioko hai na walio tangulia akhera, kwahiyo katika rakaa hii ya nne utaomba dua kwa waumini wote, na waislaamu wote na jamii nzima kwa ujumla, utasoma dua yoyote unayo ifahamu laikni kwa kiarabu.
kisha baada ya hapo imamu atatoa salaamu kama ya sala za kila siku tunazo sali majumbani na miskitini mwetu, atatoa salaamu kwa kuanzia kulia kwenda kushoto, kisha inafuata hatua nyingine ya kulichukua jeneza yaani kum-beba maiti wetu na kwenda nae kumsitiri mahala pake(kaburini mwake) inshaaallah hapo tutakua tumemaliza sala ya maiti kuanzia rakaa ya mwanzo mpaka ya mwisho.
hakuna mwanadamu alie kamilika.
coment neno lolote ambalo labda nimekosea katika mapungufu ya kibinadamu au nimesahau kipengele chochote katika mada hiyo au waweza kuandika neno lolote kutokana na ulivyo elewa mada hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
vip endapo sijui dua yoyote ya kiarabu kwa rakaa hizo mbili au nikaamua nisisome chochote je swala yangu itashih
ReplyDeleteYatakikana ujifunze akhy hiyo dua ujue kwani mtume wetu rehma na amani ziwe juu yake akutoa udhuru wa kukaa kimya... Kwa asiejua
DeleteShekh niko na Suali
DeleteInafaa wanawke kumswalia Maiti
Assalam allaykum warahmatullah wabarakatu, Allah akulipe kheri kwa darasa hili inshaallah.
ReplyDeleteBaada ya salam hakuna dua?
ReplyDeleteHakuna dua ndio
DeleteSio rakaa bali ni takbira.
ReplyDeletemasha Allah. Allah akulipeni
ReplyDeleteAmeen
DeleteDarasa nzuri mno
ReplyDeleteAllah akulipe ujira mzur kw ulichkifundisha na awalipe wote waliochukua elimu hii adhimu kw Umma wa kiislami
ReplyDeleteAmiin
جزاك الله الخير
ReplyDeleteUnanuwia vipi ukitaka kusali sala ya maiti
ReplyDeleteJazaka allahu kheri na Mola akuzidishie kwa kutufundi kumswalia maiti
ReplyDeleteMin
ReplyDeleteAsante sana ! Je ni zipi nguzo za swala ya maiti
DeleteAhsante sana kwa darasa nzuri.
ReplyDeleteMungu awabariki kwa darasa zur
ReplyDeleteJazaaka Allah Khsiran.
ReplyDeleteNa jee Maiti Ambayo imekufa kwa ajali na ikawa imepondeka pondeka je atakoshwa na kusaliwa.
ReplyDeleteجزاك الله الخير من دراستك عظيم.
ReplyDeleteUmetupa muongozo tu ila kuna wengin hawajui kutia nia Wala kumuombea dua maiti
ReplyDeleteUmetupa muongozo tu ila kuna wengin hawajui kutia nia Wala kumuombea dua maiti
ReplyDeleteKuna watu wanasalia maiti mwanamume wanamlaza mbele ya wanaosalia kichwa kushoto na mwanamke kichwa kulia. Je ni sahihi? Naomba dalili.
ReplyDeleteJe ni sharti kuwa na udhu
ReplyDeleteAssalam alaykum, warahmatullah wabarakatuh
ReplyDeleteJe swala hii ya mait kwakuwa huswaliwa wima hata kama kamvaa viatu jee inaswihi kusali bila udhu?
Ushuhuda
ReplyDeleteNilivunjika kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli nimepoteza upendo wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dk. Dawn, na kila kitu kilibadilika.
Kwa fadhili, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alinirudishia upendo ambao nilifikiri umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
Dr. Dawn kweli aligeuza machozi yangu kuwa furaha.
Dk. Dawn Anaweza Kukusaidia Na:
✅ Maneno ya mapenzi
✅ Tahadhari za Ujauzito
✅ Kurejesha Ndoa/Mahusiano
✅ Dawa za mitishamba kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Magonjwa ya Moyo, Maambukizi na mengine mengi.
📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159
Usiteseke kimya kimya. Dk. Dawn anaweza kurudisha furaha katika maisha yako!