Atakaye chunguza hali za waislamu ataona kwamba haziridhishi hata kidogo, waislamu wanategemea mataifa yasio kuwa ya waislamu katika kila jambo lao, imani zimekuwa dhaifu, waislamu wameipoteza hata sala yao. Wapo waislamu wasio sali, na hata wale wanao sali basi wengi wao hawasali kama inavyo paswa. ujinga katika mambo ya dini umeenea, uzushi umezidi, na ushirikina umekua ndio njia ya kupata riziki.
Kutokana na hayo, umoja baina ya waislamu ukaanza ukaanza kutoweka, mapenzi yakageuka kuwa bughudha na haiba yao ikaanza kupotea. Haya yote ni kwasababu ya kutofuata itikadi ilio sahihi alio kuja nayo mtume wetu muhammadi s.a.w, nayo ni itikadi ya tauhid.
maana ya Tauhidi.
kwa ufupi maana ya tauhidi ni kumpwekesha mwenyezi mungu kwa kuzielekeza ibada zote kwake yeye tu subhaanahuu wataala.
Tauhidi imegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo ni :
1) Tauhidi al Rubuubiya.
nayo ni kuamini kwamba alie umba kila kitu anae ruzuku na kuendesha mambo yote ni mwenyezi mungu asie na mshirika na pia kuamini kwamba ufalme wote ni wake. ( qurani surat Raad :16 ) na pia ushahidi mwingine soma ( qurani surat yunus : 31 ).
mwenye kuamini kwamba yupo mwingine mwenye uwezo wa kumruzuku kwa njia za ghaibu au yupo mwingine mwenye uwezo wa kumtengenezea mambo yake asie kuwa mwenyezi mungu, huyo anakuwa ametenda kitendo cha shirki al rubuubiya.
2) Tauhidi al uluuhiya.
maana yake ni kuzielekeza ibada zote kwa mwenyezi mungu subhaanahuu wataala. ( surat An am : 162-163).
kwahiyo mwenye kuelekeza ibada zake kwa asie kuwa mwenyezi mungu , kwa kusali kwenye kaburi, kuchinja kwa ajili ya mizimu, majini na mashetani, kumuogopa yoyote au chochote zaidi ya anavyo ogopwa Allah, kufuata sheria za mtu yoyote ambazo zina pingana na sheria za Allah, mtu atae fanya hayo nilio yataja na yanayo fanana na hayo basi mtu huyo atakuwa amefanya shirki ya uluuhiya.
Anae mwendea mchawi hutakiwa kuchinja mnyama kwa ajili ya kuwaridhisha majini, hupewa hirizi ambayo yalaiti kama angeweza kuzifungua na kusoma yaliomo, basi angeona na kutambua kuwa yalio andikwa humo na mchawi huyo ni mazungumzo baina ya mchawi huyo na majini kutaka wamlinde mtu huyo.
hofu za watu wa aina hii kwa wachawi hua kubwa saana kuliko hofu yao kwa mwenyezi mungu, na kuwategemea kwao wachawi hao katika kutengeneza mambo yao ni kwingi kuliko wanavyo mtegemea mwenyezi mungu, kwahiyo ana muendea mchawi au mtabiri anakuwa ametenda kitendo cha shirki Al Rubuubiya.
3) Tauhidi al asmaau wa sifaati.
Mwenyezi mungu amejipa majina mazuri mazuri na sifa nzuri nzuri na akawataka waja wake wamuombe na kumtukuza kwa majina na sifa hizo. ( quran surat Al araf : 180 ).
kwahiyo mwenye kuomba majina ya wangine wasio kuwa mwenyezi mungu kama vile kuomba kwa majina ya mitume au maswahaba au mawalii n.k, na akayaacha majina hayo matukufu ya mwenyezi mungu huyo atakuwa amefanya shirki ya Asmaau wa sifaat.
Atakae jaribu kuzigeuza sia za mwenyezi mungu na kufananisha sifa hizo ziwe sawa na sifa za binadamu au zakiumbe chochote kile, huyo pia atakuwa amefanya shirk ya Asmaau wa ssifaat.
Atakae mwendea mchawi au mpiga ramli kwa kuamini kwamba hao wachawi, au wapiga ramli au majini wana uwezo wa kutengeneza, kudhuru, kubadilisha, au kuijua elimu ya ghaibu n.k, mtu huyo atakuwa amefanya shirk ya Asmaau wa Ssifaat.
mwandishi: ulimwengu bin khatibu
email: ulimwengujuma2014@gmail.com
contact: +255656558788.
AHSANTE.
No comments:
Post a Comment