SALA YA DHUHAA.

Sala hii ni sala ya sunna alio tuusia mtume wetu muhammad s.a.w kwamba tusiache kusali sala hii kwa kadri ya uwezo wa mtu, kwasababu sala hii ina mafanikio makubwa sana duniani na akhera, mtume s.a.w amesema mola wenu amesema " Ewe bin Adam, swali rakaa 4 kwa ajili yangu mwanzo wa siku na mimi nitakutekelezea mahitaji yako kwa muda ulio baki" (imesimuliwa na Abuu daud)

                    FAIDA ZA KUSALI SALA YA DHUHAA.
1. Imesaliwa na mitume wote
2.hufuta baadhi ya madhambi unayo yajua na usio yajua.
3.Ni kama umetolea sadaqa mwili wako wote kwa ajili ya Allah.
4.Ina nguvu sana ya kuvuta riziki
5.Huchoma majini waovu
6.Inaleta ushindi mkubwa katika mambo yako mbali mbali
7.Upo mlango maalumu wa peponi kwa ajili ya wale wanao dumisha sala hii

                     MUDA WA KUSALI SALA YA DHUHAA.
Sala hii huanza kusaliwa saa 1 asubuhi hadi saa 6 mchana, na husaliwa kuanzia rakaa 2 hadi 12 kwa mwenye uwezo wa kusali rakaa zote 12 ni bora zaidi.
                                         wallahu aalam.

No comments:

Post a Comment