KUOGA
Kuoga ni nini?
Kuoga ni kuosha kiwili wili chote kuanzia juu ya kichwa hadi mwisho wa nyayo zake.
Faradhi za kuoga ni ngapi?
Faradhi za kuoga ni tatu, ambazo ni;
1.kutia nia wakati wa kuosha sehemu ya mwanzo ya kiwili wili
2.kuondosha najisi kwenye kiwili wili
3.kufikisha maji katika sehemu yote ya mwili pamoja na nywele.
Ni ipi nia ya kuoga?
Ni kusema: nanuia kuoga kwa ajili ya kuondosha hadathi kubwa,lakini nia hiyo haitakiwi itamkwe kwa ulimi ila inatakiwa iwe ndani ya moyo wako.
Ni ipi hadathi kubwa?
Hadathi kubwa ni kila yenye kuwajibisha kuoga.
Ni yepi yenye kuwajibisha kuoga?
Yenye kuwajibisha kuoga ni JANABA, HEDHI, NIFASI, KUZAA, NA KUFA.
Je, janaba ni nini?
janaba ni josho linalo patikana baada ya kugusana tupu mbili au kutokwa na manii kwa kusudia au bila kukusudia .
Nini hedhi?
Hedhi ni damu yenye kumtoka mwanamke baada ya kutimia miaka 9 kwa ajili ya uzima na ada ya kila mwezi.
nifasi ni nini?
Nifasi ni damu inayo mtoka mwanamke baada ya kuzaa.
mambo gani ni haramu kwa mwenye janaba?
Niharamu kwa mwenye janaba: kusali, kutufu, kugusa msahafu, kusoma qurani na kukaa muskitini.
Ni mambo gani ni haramu kwa mwenye hedhi na nifasi?
Ni haramu kwa mwenye hedhi na nifasi kusali, kufunga na kufanya yale yote yalio haramu kwa mwenye janaba.
wallahu aalamu.
yury's law.
No comments:
Post a Comment