Mtume s.a.w amesema :- " Dunia ni kichwa cha kila kosa"
pia kasema tena mtume s.a.w :- " Utamu wa dunia (basi ndio) uchungu wa akhera, na uchungu wa dunia (ndio) utamu wa akhera". Madhumuni ya hadithi hii ni kwamba atakae ishughulikia Dunia kwa starehe akamsahau mola wake kwa upuuzi wa dunia, basi Akhera itakuwa chungu kwake.
pia kasema mtume s.a.w :-
"Dunia ni jela ya muislamu na ni pepo ya kafiri".
Dhumuni la hadithi hii ni kueleza kwamba kafiri starehe zake ni duniani tu, ama Akhera anakwenda moja kwa moja jahannam( motoni). Ama muislamu haimstui dunia na upuuzi wake, anastahamili na kusubiri na kujiepusha na upuuzi wa dunia ili akastarehe peponi.
wallahu aalam.
No comments:
Post a Comment