JE, CONDOM NI KINGA YA UKIMWI ?

       Mara nyingi tokea kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi viongozi na vyombo mbali mbali vya habari vimekuwa vikihamasisha matumizi ya condom kwamba ndio kinga ya sahihi ya ukimwi, imefikia hatua baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini nyingine kukubaliana na jambo hili na kuhama sisha wafuasi wao juu ya matumizi ya condom.

         Sisi waislamu tunapinga kwamba condom si kinga sahihi ya ukimwi kwani mwenyezi mungu anasema " mwenye kupuza muongozo wangu kwa hakika mtu huyo ataishi maidha ya dhiki ........ qurani 20 : 124"
Aya hii inatuonesha kuwa mwanadamu hana uwezo wa kushindana na mwenyezi mungu hasa pale mwenyezi mungu anapo taka jambo lake liwe mwanadaamu hawezi kulibadili wala kulirekebisha, na kama atalazimisha kufanya hivyo yatamkuta matatizo makubwa hapa hapa duniani na kesho akhera.

Uhamasishaji wa matumizi ya condom ni dalili tosha kwamba mwanadamu anashindana na uwezo wa mwenyezi mungu kwani ukimwi ni sehemu ya adhabu ya mwenyezi mungu  kwa wanaadamu kutokana na machafu ya kumuasi mwenyezi mungu yalivyo zidi hapa duniani, ushahidi wa maneno haya ni pale mtume s.a.w aliposema katika hadithi ilio pokelewa na Abdallah ibn omary kwamba" Utakapo kithiri uchafu wa zinaa katika umma wangu ikafanywa wazi wazi basi mwenyezi mungu atawaletea gonjwa la tauni na gonjwa ambalo hawajapata kuugua watu waliopita kabla yao".

Kauli hii ni uthibitisho kuwa ukimwi ni sehemu ya adhabu ya mwenyezi mungu kwa wanaadamu kutokana na machafu yanayo fanywa hapa duniani ya zinaa, kwani ukweli usio pingika kwamba ugonjwa huu unapatikana kwa njia ya zinaa, na wazee wetu walio kufa miaka iliopita hata kabla ya uhuru hawakupata kuusikia ugonjwa huu wa ukimwi, sasa tusijidanganye kuwa balaa hili tutaweza kuliondoa au kulizuia kwa kutumia condom.

UTHIBITISHO KWAMBA CONDOM SI KINGA SAHIHI YA UKIMWI.

(A) Tokea kuingia kwa ukimwi duniani condom zilihamasishwa saana na kusambazwa kwa madai kwamba ndio kinga lakini tunacho kiona ni kwamba kila zinapo sambazwa na kutangazwa ndipo ukimwi unavyo zidi na hatujapata ripoti popote duniani kwamba condom zimeweza kupunguza au kuzuia ukimwi. kwa mfano nchi kama ETHIOPIA ni nchi pekee katika nchi ya sub-saharan africa inayo sambazwa condom saana kwa asilimia themanini ( 80% ), tokea mwaka 1994 mpaka kufikia mwaka 2000 inajumla ya walio athirika 3,000,000. kwa maana hiyo inaonekana kwamba condom si kinga ya ukimwi.

(B) Condom si kinga ya ukimwi kwa kuwa uwezo wake ni kuhifadhi uume tu lakini sehemu kubwa ya maungo ya siri ya mwanaume na mwanamke inabakia wazi, na watu wengi hasa wakati wa joto hua na michubuko sehemu za siri hasa katika katika msuguano kati ya mapaja na korodani, kwahiyo mchubuko utakao endelea wakati wa msuguano kati ya mapaja ya mwanamke na mwanaume hua ni sehemu ya maambukizo ya ugonjwa huu.

(C)Condom si kinga ya ukimwi kwa kuwa yenyewe ina matundu madogo sana ambayo huezi ukayaona kwa macho ya kawaida mpaka kwa kifaa maalumu ila ukitaka kuthibitisha kwamba condom ina matundu chukuwa maji ya pili pili alafu yajaze mai hayo ndani ya condom, alafu lamba kwa ulimi wako nje ya condom, utasikia muasho wa pili pili katika ulimi wako, kwahiyo hii inazidi kuthibitisha kwamba condom si kinga ya ukimwi.
                                 wallahu aalam.

No comments:

Post a Comment