Ndugu msomaji wa mada hii, lo ningependa kukumbushana juu ya tatizo lililopo hivi sasa duniani kuhusu janga la ukimwi. Ni gonjwa ambalo kwa hivi sasa linatishia maisha ya watu wengi duniani.
Mataifa mbali mbali, mashirika na taasisi nyingi duniani zimeuelezea ugonjwa wa ukimwi na athari zake, na mimi pia nimeonelea ni vyema niandike mada hii ili nipate kuielezea jamii juu ya gonjwa hili hatari kwa mtazamo wa kiislamu.
Huenda atakae soma na kuzingatia yaliyomo mwenyezi mungu atamuepusha na balaa hili inshaallah uislamu ni dini iliyo kamilika na nimfumo kamili wa maisha ya wanadamu, bila shaka jamii inategemea uislamu pekee ndio utakao toa ufumbuzi wa matatizo yote duniani ikiwemo suala la ukimwi. Kwa atakae kubali na kufuata kwa kuangalia mafundisho ya Qurani na hadithi za mtume huyo pekee ndio atakae nusurika na janga hili.
UKIMWI NI NINI ?
Ukimwi ni ugonjwa ambao unadhoofisha kinga ya mwili wa mwanadaamu. Vijidudu vya human immuno deficiency virus ( HIV ) vikisha ingia mwilini hushambulia chembe hai nyeupe ( white blood cells ) ambayo humsaidia mwanadamu kupambana na maradhi mwilini mwake.
Pia chembe hai nyeupe ( white blood cells ) vikishirikiana na chembe hai nyekundu ( red blood cells ) kwa pamoja huunda damu katika mwili wa mwanaadamu. Hivyo basi chembe hai nyeupe zikimalizika mwilini kutokana na kushambuliwa na HIV basi mwili huo hukosa kinga kiasi ambacho ugonjwa wowote utapoingia mwilini mgonjwa atateseka mpaka kufa hata kama atatumia dawa kwasababu dawa pekee haiwezi kufanya kazi mpaka ishirikiane na chembe hai nyeupe.
Tumeshuhudia mara nyingi wagonjwa wa ukimwi mwisho wao hufa kwa njia mbalimbali wengine hutokwa na vidonda vingi mwilini na wengin hukohoa sana kama wagonjwa wa kifua kikuu na wengine kuharisha sana kama wagonjwa wa kipindupindu na njia zingine mbalimbali.
HALI YA UKIMWI DUNIANI
Ugonjwa wa ukimwi uliripotiwa kwa mara ya kwanza marekani mwaka 1981 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 1998 zaidi ya watu wazima millioni 33 ambao kati yao watoto ni million 4, na millioni 1.2 ni wenye umri chini ya miaka 15 wanaishi na virus vya ukimwi Duniani.
Mwaka 1998 vijana millioni 3 wenye umri kati ya miaka 15-24 waliambukizwa virusi vya ukimwi, hivyo ni wastan wa vijana watano wanaambukizwa kila dakika.
Hali ya ukimwi Tanzania tangu ugonjwa huu ufahamike hapa nchini mwaka 1983 ambapo wagonjwa watatu waligunduliwa, kumekuwepo na ongezeko la wagonjwa mwaka hadi mwaka mpaka kufikia 1997 wagonjwa 103,185 wameripotiwa katika hospitali mbalimbali nchi nzima.
Tanzania imeshika nafasi ya sita katika nchi za sub-saharan Africa zikiongozwa na africa kusini yenye waathirika 4,200,000 na ya pili ni ethiopia yenye waathirika 3,000,000 na ya tatu ni nigeria yenye waathirika wa ukimwi 2,700,000 na nchi ya tano ni zimbabwe yenye waathirika 1,500,000 na nchi ya ni tanzania yenye waathirika 1,300,000. hiyo ni record ya mwaka 2000, sasa jiulize wewe mwenyewe kama mwaka 2000 nchi ya tanzania ilikuwa nafasi ya sita je, mpaka leo mwaka 2017 tanzania itakuwa nafasi ya ngapi??
UNAPATIKANAJE UKIMWI ?
Ukimwi unapatikana kwa kuwambukizwa na mtu alie athirika na virusi vya HIV vinavyo sababisha ukimwi kupitia ngono au kushirikiana katika matumizi ya vifaa vyenye ncha kali kama nyembe, sindano na vinginevyo. kwakua virusi vya ukimwi hupatikana katika maji maji ya mwili kama vile damu, usaha, maziwa ya mama, shahawa, na maji maji ( ute ) utokao ukeni kwa mtu alie ambukizwa virusi vya ukimwi, hata hivyo damu na maji maji ( ute ) yatokanayo na tendo la ngono ndio yanaidadi kubwa ya virusi vya ukimwi ukilinganisha na maji maji mengine ya mwili. wakati wa kufanya tendo la ngono virusi vya ukimwi vinaweza kujipenyeza kutoka katika damu au maji maji ( ute ) au shahawa ya mtu mwenye uambukizo hadi katika damu ya mtu mwingine kwa kupitia ngozi laini ya uke au uume au njia ya haja kubwa.
Sisi waislamu tuna sema Ukimwi unaenezwa zaidi kwa njia ya zinaa kwasababu neno ngono halitenganishi kati ya wenye ndoa na wasio na ndoa, hivyo basi ndoa sahihi ya kiislamu iliyo fuata maadili na yenye kulinda mipaka yake ipasavyo, ngono kati yao haiwezi kuwa sababu ya kuambukizana ukimwi, isipokuwa ni baada ya kuvunjwa mipaka na maadili ya ndoa hiyo, kwahivyo tunasema ukimwi unasababishwa na kuenezwa sana kwa wanaadamu duniani kwa njia ya zinaa.
Zinaa ni jambo baya sana na ndio maana sheria ya kiislamu ina muhukumu mzinifu alie kwisha oa au kuolewa hukumu ya kifo. Hukumu hii inaonesha uwezo wa mwenyezi mungu katika kuyajua mambo yalio jificha kwa kuwa hukumu hii hasa kwa wakati huu wa ukimwi ndio njia pekee ya kuwanusuru baadhi ya wenye ndoa kwani mke au mume akivunja mipaka ya ndoa ( akizini ) na akibainika akauwawa hikima yake ni kwamba zinaa hiyo imemsababishia ugonjwa wowote ( wazinaa) asije mwambukiza mwenziwe, hii ni kuonyesha uislamu ulikwisha weka zamani mazingira ya kupambana na magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi kutokana na sheria zake.
Njia nyingine inayo sababisha maambukizo ya ukimwi ni katika makundi au vijiwe vya watumia madawa ya kulevya kwa kushirikiana sindano wanazo dungiwa dawa hizo, kwa kawaida vijana watumiao dawa za kulevya hudungwa sindano vijiweni na sindano moja hutumika kudunga vijana wengi hali inayo sababisha kuambukizana virusi vya ukimwi kama kuna muathirika miongoni mwao.
Na ndio maana mwenyezi mungu akakataza vilevyi vyote ili heshima ya mwanaadamu iweze hifadhika na kumuhifadhi na magonjwa mengin tunayo yajua na tusio ya jua. hii ni sehemu fupi ya ukimwi katika uislamu na tutazidi kufahamishana kadri mwenyezi mungu atavyo tuwezesha.
waallahu aalam.
No comments:
Post a Comment