Ndugu zangu katika masahaba wa mtume s.a.w wamegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambazo ni answaar na muhajiriina, kwahiyo pindi alipo kufa mtume s.a.w wakaona answaari wazungumzie ukhalifa wa baada ya mtume.
Akasimama Saad ibn Ubada akazungumza na answar wenzake na kuwakumbusha fadhila za answar katika maisha ya mtume mpaka mtume s.a.w akasema" kama watu watafuata njia hii na answar wakafuata njia nyingine basi mimi mtume nitafuata njia ya answari", Saadi akazidi kuwakumbusha wenzie jinsi mtume alivyo kuwa anatupenda( answar ) kwahiyo tunahaki sisi ya kuwa viongozi baada ya mtume kuondoka.
Maongezi hayo yalikuwa yanafanyika katika jumba la banii saida,kwahiyo kipindi answar wakiendelea na mazungu mzo hayo baadhi ya muhajiriin hawakuwako katika eneo hilo la mazungumzo kama vile omar na abuu bakr, basi omar na abuu bakar walivyo pata taarifa kuwa kuna semina inayo endelea kufanyika katika jumba la banii saida wakawahi kwenda kusikiliza mazungumzo hayo, wakafika pale na kuona watu wanapanga kuhusu mambo ya uongozi baada ya mtume, lakini kipindi hicho hata mwili wa mtume ulikuwa haujazikwa.
Na hapa mayahudi walipata mdomo na kusema kuwambia waislamu kwamba " hakuna watu wabaya kama waislaamu, yaani hamjamzika mtume wenu mnaanza kugombania uongozi" walikuwa wakimwambia maneno hayo ally ibn abii twalib na ally ibn abii twalib akawajibu akawaambia " bora sisi waislamu tunagombea kumpata kiongozi atakae kuwa anatuongoza sisi katika mambo ya dini na dunia, ili hata katika mazishi ya mtume wetu tumsikilize yeye amiri wetu, kuliko ninyi mayahudi, pindi mungu alipo wapitisha katika bahari na akawaangamiza firauni na majeshi yake huku mnashuhudia lakini mlipo fika nchi kavu hata kabla maji hayaja kauka katika nyayo zenu, mnamwambia mussa, eewee mussa tutengenezee mungu wa sanamu kama walio kuwa wanaabudu babu zetu, huyo mnaetaka mtengenezewe ni nani na huyo alie waokoeni katika bahari ni nani? kwahiyo ally akawambia kati ya sisi na ninyi ni wapi wenye madhambi? mayahudi kwa jeuri yao hawakujibu swali hilo
Kwahiyo baada ya muda mfupi Abuu bakari akasimama katika semina hiyo na kuwapongeza answar kwa kile walicho kifanya na kuwaambia ni kweli mtume aliwapenda sana answar, hakuacha sifa abuu kakri ya answar siku hiyo ila zote alizitaja kisha akazitaja na sifa zote za muhaajiriin, lakini akawakumbusha kauli ya mtume alio bashiri kwamba" ni lazima kiongozi wenu atoke kwa makurayshi " na mtume alikuwa akilionyesha hilo mara mara, sasa mimi kama abuu bakri rai yangu ni kwamba amiri wetu atoke kwa makurayshi na mawaziri watoke kwa answar.
Baada ya rai hiyo ya abuu bakri, akasimama bwana mmoja anaitwa ubabu ibn mundhir akasema" haiwezezekani kisha ubabu akazidi kupaza sauti na kusema enyi watu wa answar ikiwa hao muhajiriin watapinga sisi kutupa uamiri na kutaka tuwe mawaziri basi lengo letu tunawaambia sisi (answar ) tuwe na amiri wetu na wao (muhajiriin) wawe na amiri wao.
Kisha baada ya hapo akasimama omary ibn khatwaab, akamwambia abuu ubabu kwamba watu wawili hawawezi kuongoza katika umma mmoja, kwahiyo bora apatikane mmoja alafu huyo mwingine awe waziri wake.
Kisha akasimama tena abuu ubabu ibn mundhir na kusema " enyi answar msiachilie kabisa suala hili, kama wamekataa suala la kuwa na sisi viongozi na wao viongozi basi nakwambieni answar kamateni hapo hapo,mkija mkakosea kidogo watakuja wachukue nafasi hii na heshima yenu ikakosekana.
kisha baada ya hapo akasimama bwana mmija anaitwa abuu ubeida ibn jarrah akasema," enyi watu wa answar nyie ndio watu wa mwanzo kumnusuru mtume, basi msiwe watu wa kwanza kusababisha fitna na chuki katika uislamu.
Kisha akasimama mmoja katika answar anaitwa bashiir ibn saad akasema, " enyi watu muhammad alikua ni mkureyshi katika kabila tukufu la maka na wale walio kuja nae kutoka makka, sisi tuka watukuza na kuwa kirimu mpaka tukapata heshima alio tupa mtume, basi na wao pia wanahaki ya kuwa nyuma ya mtume katika uongozi kuliko sisi, kama tumetangulia na kuzidi kuzidi kutangulia katika uislamu na tuka wanusuru ndugu zetu waislamu na tukapigana jihad mbali mbali katika uislamu, tumefanya hivyo kwa ajili ya kupata radhi za mwenyezi mungu, hatukufanya hivyo ili tuje tupate uongozi leo, kwanini magombania uamir?, kwanini tusisikilize viongozi ( muhajiriin ) wanavyo tuambia tukafuata ili tuzidi kupata kheri zaidi?
Alipo sema hayo wote wakanyamanza, pale pale akasimama abuu bakri na kukamata mkono wa omary na kuuinua juu, kisha akakamata mkono wa abuu ubeida na kuuinua juu akasema " mimi nimekuridhieni watu wawili hawa, chagueni mtu mmoja kati ya hawa awe amiri wetu.
omari akarudi nyuma na kusema " ewee abuu bakri mimi bora nipeleke kichwa changu kikatwe kuliko kuwa amiri mbele yako, wewe abuu bakri ndio unahaki ya kuwa khalifa kwasababu mtume alipo taka kutuongoza katika jambo lolote la dini alisema abuu bakri atuongoze awe imamu wetu, kama mtume karidhika abuu bakri atuongoze katika jambo la dini yetu kwanini sisi tusiridhike abuu bakri atuongoze katika jambo la dunia, wakati wa sala mtume amesema abuu bakri ndio asalishe, hi inaonesha mtume alitaka abuu bakri ndio awe kiongozi baada yake.
Omary alipotaka kuunyanyua mkono wa abuu bakri, yule answar ( bashiir ibn saad ) akawa yeye wa kwanza kuinua mkono wa abuu bakri kabla ya omary, kisha akafuata omary akainua mkono wa abuu bakri juu, kisha akafuata abuu ubeida kisha answar wote pamoja na muhajiriin wote walio kuwako pale wakasimama kwa ishara ya kwamba wameridhia abuu bakri kuwa kiongozi wao. yaani wote answar na muhajiriin wameridhia abuu bakri awe khalifa wao, neno amiril-muuminina halikuwako wakati huo kwasababu amiril-muuminiina limeanza wakati wa omary ibn khatwab, hapa alikuwa anajulikana kama khalifatu-rasuuli llah.
hapo ndipo uongozi rasmi wa abuu bakri ulipo anza na kuwa kalifa wa kwanza katika uislamu.
wallahu aalam.
No comments:
Post a Comment