ABDU ROGO.TAFSIRI YA SURAT-TAUBA. 5

ABDU ROGO.TAFSIRI YA SURAT-TAUBA. 3

ABDU ROGO.TAFSIRI YA SURAT-TAUBA. 2

TAKWIMU YA QURAN

            TAKWIMU YA QUR-AANI TUKUFU.

Qurani tukufu ni kitabu cha pekee cha mwenyezi mungu alicho mteremshia mtume Muhammad s.a.w ambacho kimebaki na kitaendelea kubaki bila kuongezwa au kupunguzwa sura, aya, neno, au hata herufi yake moja. Kwa mujibu wa idadi iliyo tolewa na sheikh Bahai katika kitabu chake kiitwacho al-kashkuw, qurani ni kitabu chenye jumla ya sura 114, aya6236, maneno 76,440 na herufi 322,373.

Idadi ya kila herufi katika Qurani ni hii;
1. ALIF     40,792
2.BAA       1,140
3.TAA       1,299
4.THAA    1,291
5.JIIM       3,293
6.HAA    9,997
7.KHAA    2,419
8.DAAL      10,903
9.DHAAL    4,840
10.RAA        10,903
11.ZAA           9,583
12.SIIN        4,091
13.SHIIN     20,133
14.SAAD      1,274
15.DHAAD    1,200
16.TWAA      840
17.DHWAA     9,220
18.A,AYNI      7,499
19.A,GHAYNI    1,120
20.FAA            8,497
21.QAAF        5,240
22.KAAF        2,500
23.LAAM      26,019
24.MIIM     20,560
25.NUUN        20,360
26.WAAW        13,700
27.HEE(HAA)    700
28.YAA(YEE)     502

          WALLAHU AALAM*******YURY'S LAW

HIJJA

                           ELIMU YA HIJJA

Hijja ni nini?
Hijja ni kuikusudia nyumba ya mwenyezi mungu (ilioko makka) kwa ajili ya mambo ya hijja (Nusuki)

Ni mambo yepi hayo (Nusuki)?
Mambo hayo ni vitendo vyote vya hijja kama vile nguzo zake na wajibu wake.

Nguzo zake ni ngapi?
Nguzo za hijja ni tano, ambazo ni;
1.ni kuhirimia pamoja na kutia nia 
2.kusimama Arafa
3.kutufu( kuizunguka ) Al-ka'ba mara saba
4.kwenda baina safa na mar-wa mara saba
5.kunyoa au kupunguza nywele za kichwani.

Wajibu wa hijja ni mambo mangapi?
wajibu wa hijja ni mambo matano, ambayo ni ;
1.Kuhirimia katika kituo
2.kurembea magino matatu
3.kupitiwa na usiku ( kulala) muzdalifa.
4.kupitwa na usiku (kulala) mina siku za mwezi 11, 12 na 13 za mfungo tatu
5.Tawafu ( kuizunguka Al-ka'ba ) kwa kuaga kwa anae ondoka makka

Ni mambo mangapi hua haramu baada ya kuhirimia?
mambo kumi hua ni haramu kwa mtu alie hirimia,
1.kuvaa nguo ilio shonwa
2.kufunika kichwa kwa mwanamme na kufunika uso kwa mwana
3.kuchana nywele au kuzitia mafuta
4.kunyoa nywele
5.kukata kucha
6.kujipamba au kujitia manukato
7.kumuua mnyama kwa kumuwinda
8.ndoa
9.kufanya tendo la ndoa
10.kukumbatiana kwa matamanio

        WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.

FUNGA.

                    ELIMU YA FUNGA.

Funga ni nini?
Ni kujizuilia na kula na kunywa, kuingilia/ au kuingiliwa (kufanya tendo la ndoa) na kila jamboleny kufuturisha kuanzia inapo chomoza alfajiri mpaka linapo zama jua, kwa siku zote za mwezi wa Ramadhani.

Ni nani anawajibika kufunga?
Ni wajibu kwa kila muislamu aliye baleghe, mwenye akili timamu, anaye weza (huko kufunga ) na alie toharika kutokana na hedhi na nifasi.

Faradhi za funga ni ngapi?
Faradhi za funga ni mbili;
1. nia
2.ni kujizuilia na yenye kufuturisha  ( yenye kufunguza)

Ni yepi hayo yenye kufuturisha?
Ni kila jambo lenye kubatilisha funga, nayo ni mambo manane;
1.kuingiza kitu ndani kwa makusudi (katika tundu za mwili)
2.kujitapisha kwa makusudi
3.kupatwa na hedhi
4.nifasi
5.kujitoa manii kwa makusudi
6.kufanya tendo la ndoa
7.kuritadi (kutoka katika uislaamu)
8.kuwa na wazimu

Ni siku zipi haramu kufunga?
siku hizo ni
1.siku za Idd mbili ( Idil-fitri na Idil-hajj)
2.siku za mwezi 11, 12 na 13 katika mfungo tatu 
3.siku ya shaka, isipokuwa itapo wafikiana na ada yake ( ya kufunga katika siku hiyo) au kuunganisha na funga ilio kabla yake.

           WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.

ZAKATUL-FITRI

                                 ZAKATUL-FITRI

Zakatul-fitri ni nini?
Ni vibaba vinne vya chakula (kinacho pendwa sana) katika mji.

Ni nani anae wajibika kutoa Zakatul-fitri?
Anae wajibika kutoa zakatul-fitri ni kila muislamu alie huru ambae ana ziada katika chakula chake( cha siku ya Idd) kwa ajili yake yeye na walio mlazimu yeye kuwalisha miongoni mwa waislamu. Na atatoa kwa ajili yake, na pia awatolea wale waislamu . yeye kuwalisha miongoni mwa waislamu.

Ni wakati gani ni wajibu kutoa zakatul-fitri?
Zakatul-fitri hutolewa kuanzia magharibi ya siku ya mwisho wa Ramadhani.

   WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.

ZAKA.

                                            SOMO LA ZAKA.
Nini maana ya zaka?
Zaka ni kutoa kiwango maalumu cha mali mahsusi na kuwapa wanaopasa (kuwapa hiyo zaka) katika mbea nane au mbea moja miongoni mwa hizo.

Ninani hao mbea nane wanaopasa(kupewa zaka)
Hao ni wale walio tajwa katika qurani, kwa kauli yake mwenyezi mungu katika surat Tauba aya ya 60, amesema Allah" sadaka hupewa (watu hawa) ; mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanao tiwa nguvu nyoyo zao (juu ya uislamu) na katika kuwapa uungwana watumwa na katika kuwasaidia wenye deni na kwa ajili ya mwenezi mungu na msafiri alie haribikiwa "

Ni wepi hao mafakiri?
Hao ni wale ambao hawana mali wala chumo linalo watosheleza kwa haja zao za lazima.

Ni wepi hao masikini?
Hao ni wale wenye mali au chumo lakini hawajitoshelezi kwa haja zao za lazima.

Ni wepi hao wanao ifanyia kazi zaka?
Hao ni wale wanao kusanya zaka na kuigawa kwa wanao pasa (kupewa zaka)

Ni wapi hao wanao tiwa nguvu nyoyo zao (juu ya uislamu)?
ni wale walio silimu karibu.

Ni wepi hao wenye kupewa uungwana?
Ni wale watumwa walio andikwa( kuachwa huru ).

Ni nani hao wenye madeni?
Hao ni wale wenye madeni ambayo hawawezi kuyalipa.

Ni wepi hao walio katika njia ya mwenyezi mungu?
Ni wale wanao jitolea katika njia ya mwenyezi mungu ( kwa ajili ya kutaka radhi za mwenyezi mungu)

Ni wepi walio haribikiwa njiani?
Hao ni wasafiri ambao hawasafiri kwa ajili ya maasi na hawana mali inayo watosheleza katika safari yao.

Ni kitu gani kilicho wajibu kukitolea zaka?
ni wajibu kwa: 1.wanyama wanao fugwa(ambao ni halali)
                        2.dhahabu na fedha
                       3.vipando
                      4.matunda
                     5.mali ya biashara

Ni wepi wanyama hao?
Hao ni ng'ombe, mbuzi, na kondoo, nyati na ngamia .

Nini shuruti za wanyama hao?
shuruti za wanyama hao ni Nisab, Sawm na Hawli

Nisab ni nini?
Ni kipimo maalumu cha kisheria

Sawm ni nini?
Ni kula wanyama hao katika ardhi isiyo milikiwa na mtu yeyote.

Hawli ni nini?
Huko ni kupita mwaka mmoja kamili.

Nini shuruti za zaka ya dhahabu na fedha, na mali ya biashara?
Shuruti zake ni Nisab na Hawli.

Ni matunda gani ambayo hutolewa zaka?
matunda ambayo hutolewa zaka ni Tende na Zabibu

Ni vipando gani ambavyo hutolewa zaka?
Ni kila kinacho liwa kama Mchele na Ngano.

Ni nini shuruti za zaka ya vipando na matunda?
Ni Nisab tu ( kufikia kiwango maalum)

      WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.

SALA YA JENEZA.

                                SALA YA JENEZA (SALA YA MAITI)

Mambo gani ni wajibu kufanyiwa maiti?
Ni wajibu kufanyiwa matayarisho, nayo ni;
        1.kukoshwa
        2.kukafiniwa
        3.kusaliwa
        4.kuzikwa.

Vipi husaliwa sala ya maiti?
1.Anuilie anaesali  kuwa anamsalia huyo maiti pamoja na kupiga takbir-Allahu akbar
2.ASome suratil faatiha
3.Aseme Allahu Akbar
4.Amsalie mtume S.a.w
5.Aseme Allahu akbar
6.Amwombee dua maiti
7.Aseme Allahu Akbar
8.Atoe salamu

             WALLAHU AALAM*******YURY'S LAW