ELIMU YA HIJJA
Hijja ni nini?
Hijja ni kuikusudia nyumba ya mwenyezi mungu (ilioko makka) kwa ajili ya mambo ya hijja (Nusuki)
Ni mambo yepi hayo (Nusuki)?
Mambo hayo ni vitendo vyote vya hijja kama vile nguzo zake na wajibu wake.
Nguzo zake ni ngapi?
Nguzo za hijja ni tano, ambazo ni;
1.ni kuhirimia pamoja na kutia nia
2.kusimama Arafa
3.kutufu( kuizunguka ) Al-ka'ba mara saba
4.kwenda baina safa na mar-wa mara saba
5.kunyoa au kupunguza nywele za kichwani.
Wajibu wa hijja ni mambo mangapi?
wajibu wa hijja ni mambo matano, ambayo ni ;
1.Kuhirimia katika kituo
2.kurembea magino matatu
3.kupitiwa na usiku ( kulala) muzdalifa.
4.kupitwa na usiku (kulala) mina siku za mwezi 11, 12 na 13 za mfungo tatu
5.Tawafu ( kuizunguka Al-ka'ba ) kwa kuaga kwa anae ondoka makka
Ni mambo mangapi hua haramu baada ya kuhirimia?
mambo kumi hua ni haramu kwa mtu alie hirimia,
1.kuvaa nguo ilio shonwa
2.kufunika kichwa kwa mwanamme na kufunika uso kwa mwana
3.kuchana nywele au kuzitia mafuta
4.kunyoa nywele
5.kukata kucha
6.kujipamba au kujitia manukato
7.kumuua mnyama kwa kumuwinda
8.ndoa
9.kufanya tendo la ndoa
10.kukumbatiana kwa matamanio
WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.
No comments:
Post a Comment