ELIMU YA FUNGA.
Funga ni nini?
Ni kujizuilia na kula na kunywa, kuingilia/ au kuingiliwa (kufanya tendo la ndoa) na kila jamboleny kufuturisha kuanzia inapo chomoza alfajiri mpaka linapo zama jua, kwa siku zote za mwezi wa Ramadhani.
Ni nani anawajibika kufunga?
Ni wajibu kwa kila muislamu aliye baleghe, mwenye akili timamu, anaye weza (huko kufunga ) na alie toharika kutokana na hedhi na nifasi.
Faradhi za funga ni ngapi?
Faradhi za funga ni mbili;
1. nia
2.ni kujizuilia na yenye kufuturisha ( yenye kufunguza)
Ni yepi hayo yenye kufuturisha?
Ni kila jambo lenye kubatilisha funga, nayo ni mambo manane;
1.kuingiza kitu ndani kwa makusudi (katika tundu za mwili)
2.kujitapisha kwa makusudi
3.kupatwa na hedhi
4.nifasi
5.kujitoa manii kwa makusudi
6.kufanya tendo la ndoa
7.kuritadi (kutoka katika uislaamu)
8.kuwa na wazimu
Ni siku zipi haramu kufunga?
siku hizo ni
1.siku za Idd mbili ( Idil-fitri na Idil-hajj)
2.siku za mwezi 11, 12 na 13 katika mfungo tatu
3.siku ya shaka, isipokuwa itapo wafikiana na ada yake ( ya kufunga katika siku hiyo) au kuunganisha na funga ilio kabla yake.
WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.
No comments:
Post a Comment