SOMO LA ZAKA.
Nini maana ya zaka?
Zaka ni kutoa kiwango maalumu cha mali mahsusi na kuwapa wanaopasa (kuwapa hiyo zaka) katika mbea nane au mbea moja miongoni mwa hizo.
Ninani hao mbea nane wanaopasa(kupewa zaka)
Hao ni wale walio tajwa katika qurani, kwa kauli yake mwenyezi mungu katika surat Tauba aya ya 60, amesema Allah" sadaka hupewa (watu hawa) ; mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanao tiwa nguvu nyoyo zao (juu ya uislamu) na katika kuwapa uungwana watumwa na katika kuwasaidia wenye deni na kwa ajili ya mwenezi mungu na msafiri alie haribikiwa "
Ni wepi hao mafakiri?
Hao ni wale ambao hawana mali wala chumo linalo watosheleza kwa haja zao za lazima.
Ni wepi hao masikini?
Hao ni wale wenye mali au chumo lakini hawajitoshelezi kwa haja zao za lazima.
Ni wepi hao wanao ifanyia kazi zaka?
Hao ni wale wanao kusanya zaka na kuigawa kwa wanao pasa (kupewa zaka)
Ni wapi hao wanao tiwa nguvu nyoyo zao (juu ya uislamu)?
ni wale walio silimu karibu.
Ni wepi hao wenye kupewa uungwana?
Ni wale watumwa walio andikwa( kuachwa huru ).
Ni nani hao wenye madeni?
Hao ni wale wenye madeni ambayo hawawezi kuyalipa.
Ni wepi hao walio katika njia ya mwenyezi mungu?
Ni wale wanao jitolea katika njia ya mwenyezi mungu ( kwa ajili ya kutaka radhi za mwenyezi mungu)
Ni wepi walio haribikiwa njiani?
Hao ni wasafiri ambao hawasafiri kwa ajili ya maasi na hawana mali inayo watosheleza katika safari yao.
Ni kitu gani kilicho wajibu kukitolea zaka?
ni wajibu kwa: 1.wanyama wanao fugwa(ambao ni halali)
2.dhahabu na fedha
3.vipando
4.matunda
5.mali ya biashara
Ni wepi wanyama hao?
Hao ni ng'ombe, mbuzi, na kondoo, nyati na ngamia .
Nini shuruti za wanyama hao?
shuruti za wanyama hao ni Nisab, Sawm na Hawli
Nisab ni nini?
Ni kipimo maalumu cha kisheria
Sawm ni nini?
Ni kula wanyama hao katika ardhi isiyo milikiwa na mtu yeyote.
Hawli ni nini?
Huko ni kupita mwaka mmoja kamili.
Nini shuruti za zaka ya dhahabu na fedha, na mali ya biashara?
Shuruti zake ni Nisab na Hawli.
Ni matunda gani ambayo hutolewa zaka?
matunda ambayo hutolewa zaka ni Tende na Zabibu
Ni vipando gani ambavyo hutolewa zaka?
Ni kila kinacho liwa kama Mchele na Ngano.
Ni nini shuruti za zaka ya vipando na matunda?
Ni Nisab tu ( kufikia kiwango maalum)
WALLAHU AALAMU*******YURY'S LAW.
Harrah's Atlantic City - MapyRO
ReplyDeleteFind addresses, phone numbers, and reviews 남양주 출장샵 for 경상남도 출장안마 Harrah's Atlantic City in Atlantic City, NJ. Check out the map and the area's 인천광역 출장마사지 map of Atlantic 화성 출장안마 City to 강릉 출장마사지 see