NAJISI

Najisi ni zipi?
Najisi ni damu, usaha, matapishi, ulevi, mbwa, nguruwe, na maziwa ya mnyama isiyo liwa nyama yake na chenye kutoka kwenye njia mbili( tupu mbili ) isipo kuwa manii kwani hayo ni ( tohara ) na maiti, manyoya yake na mifupa yake ( vyote ni najisi ) isipokuwa maiti ya binaadamu, samaki na nzige.

vipi hutoharika najisi?
nijisi hutoharishwa kwa kukoshwa mahala ilipo ingia najisi kwa maji yalio tohara mpaka iondoke harufu yake na rangi yake na ladha yake ( isipo kuwa najisi ya mbwa na nguruwe na ngozi ya maiti)

Vipi hutahirika najisi ya mbwa na nguruwe?
Najisi ya mbwa na nguruwe hutahirika kwa kukoshwa mahala ilipo kuwa najisi mara saba, moja kati ya hizo kwa mchanga.

Vipi hutoharika ngozi ya maiti?
Ngozi ya maiti hutoharika kwa kudubaghiwa ( kukaushwa ).
                                                yurys law. 
                                         WALLAHU AALAM.


No comments:

Post a Comment