Tohara ni nini?
tohara ni kitendo ambacho haitosihi sala pasi na kukifanya kama kuondosha najisi, kustanji, kutawadha, kukoga(josho), kutayammam.
Njia za tohara ni zipi?
Njia za tohara ni maji, mchanga, jiwe, kudubaghi( kukausha) kama ngozi na (sabuni)
Niyepi maji ambayo yanafaa kujitoharishia?
Ni kila maji ambayo huteremka kutoka mawinguni au yanayotoka(bubujika) ardhini yasiyo najisi wala yaliotumiwa.
Niyepi maji yaliyo najisika?
Ni maji yaliyo kidogo ambayo yameingia najisi ndani yake.
Ni yepi maji yalio tumika?
Ni maji kidogo yalio tumiwa katika kuondosha hadathi au najisi.
Ni yepi maji kidogo?
Ni maji yasiyo timia kulla mbili
Ni yepi maji mengi?
Ni maji yaliyo timia kulla mbili na zaidi.
Ni nini kulla mbili?
Kulla mbili ni maji yaliyo kiasi cha wakia 148 au yaliyo katika sehemu ambayo huenea birika la maji lenye pembe nne lenye urefu wa dhiraa moja na robo kwa marefu ya kwenda juu na mapana ya kwenda chini ( urefu wa kwenda chini).
wallahu aalamu.
No comments:
Post a Comment