SALA.

                                                MAFUNDISHO YA SALA.

Nani inamlazimu sala?
Sala humlazimu kila muislamu alie baleghe, mwenye akili timamu, na ni juu ya waliii wa mtoto(mzee)kumuamrisha kusali baada ya kutimia umri wa miaka saba na kumpiga pindi akiwacha(kusali)baada ya kutimia umri wa miaka kumi.

sharti za sala ni ngapi?
sharti za sala ni tano, ambazo ni;
    1.kujitaharisha(kwa kuepukana)na hadathi kubwa na ndogo .
    2.kutahirika kwa kiwili wili,nguo na pahala pa kusalia(kutokana) na najisi.
    3.kustiri utupu.
     4.kujua kuingia kwa wakati.
     5.kuelekea kibla.

Idadi ya rakaa za witri ni ngapi?
Idadi ya rakaa za witri ni kumi na moja na wakati wake ni baada ya sala ya insha hadi kuchomoza alfajiri.

Nyakati ngapi hua ni haramu kusali?
Hua ni haramu kusali katika nyakati tano, ambazo ni :
      1.wakati wa kuchomoza jua mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki.
      2.wakati jua linapokuwa lipo sawa sawa na kitu(saa sita) isipokuwa siku ya ijumaa, mpaka lipinduke jua.
      3.wakati jua linapo kuwa manjano mpaka linapo kuchwa( magharibi).
      4.baada ya sala ya alfajiri mpaka lichomoze jua.
      5.baada ya sala ya alaasiri mpaka lichwe jua.

Nguzo za sala ni ngapi?
Nguzo za sala ni kumi na nne.ambazo ni
   1.kusimama kwa anae weza katika sala ya faradhi.
   2.nia
   3.takbiratul ihram
   4.kusoma suratil faatiha
   5.kurukuu
   6.kujituliza( katika rukuu, itidali na sijda)
   7.itidali
   8.kusujudu
   9.kukaa kitako baina ya sijda mbili
  10.kukaa kitako kwa ajili ya tahiyatu ya mwisho
  11.tahiyatu ya mwisho
  12.kumsalia mtume katika tahiyyatu ya mwisho
  13.salamu ya kwanza
  14.utaratibu ( kwa mpangilio wake huu kuanzia nguzo ya 1-13)

**itidali ni kisimamo baada ya kutoka katika rukuu kabla ya kusujudu.

Ni zipi sunna za sala kabla yake
Sunna za kabla au nje ya sala ni Adhana na Iqama.

Ni zipi sunna za ndani ya sala?
Sunna za ndani ya sala zipo aina mbili ambao ni ; Ab'adh na hay-ati

Sunna za Ab'adh za sala ni ngapi?
Sunna hizo ni tatu, ambazo ni ;
     1.Tahiyyatu ya kwanza
     2.kumsalia mtume katika tahiyyatu ya kwanza
     3.kunuti katika sala ya asubuhi na katika sala ya witri kwenye nusu ya pili ya mwezi wa ramadhani
   
Sunna za hay-ati ni ngapi?
Sunna za hay-ati ni kumi na tano , ambazo ni ;
    1.kunyanyua mikono miwili sawa na mabega wakati wa takbiratul ihram, wakati wa kurukuu, wakati wa itidali, na wakati wa kusimama kutoka katika tahiyyatu ya kwanza.
    2.kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua au juu ya kitovu.
    3.Dua ya kufungulia sala
    4.kusoma " Audhu billahi minashaytani......
    5. kuitika Amin
    6.kusoma sura baada ya suratil faatiha katika rakaa ya kwanza na ya pili
    7.kudhihirisha sauti katika mwahala mwake na kutodhihirisha sauti  mwahala mwake.
    8.kusema Allahu akbar wakati wa kuinama ( kwenda katika rukuu) na wakati  wa kunyanyuka.
    9.kusema samiallahu liman hamidah katika itidali
   10.kusema sub-haana rabbial Adhiym katika rukuu mara tatu, na kusema sub-haana rabiyal A'la katika sijda mara tatu.
    11.kuweka mikono miwili juu ya mapaja hali ya kuukunjua mkono wa kushoto na kuukunja wa kulia isipokuwa kidole cha shahada.
     12.kuukalia mguu wa kushoto ( katika vitako vilivyomo katika sala)
     13.kuupitisha mguu wa kushoto utokezee kuliani ( na kulikalia tako la kushoto ) katika tahiyyatu ya mwisho.
     14.salamu ya pili
     15.Nia ya kutoka katika sala

Ni yepi mambo yenye kubatilisha sala?
Mambo yenye kubatilisha sala ni manne,ambayo ni ;
    1.kusema kwa kukusudia
    2.kufanya vitendo vitatu mfululizo
    3.kula au kunywa
   4.kuacha nguzo miongoni mwa nguzo za sala au kukosa shuruti miongoni mwa shuruti za sala.

Ninini hukumu ya alie acha nguzo ya sala kwa kusahau?
Ataileta nguzo hiyo atakapo ikumbuka na atasujudu " sijdatis-sahwi"

Ninini hukumu ya alie acha sunna kwa kusahau?
hatailipa sunna hiyo bali atasujudu sijidatus-sahwi

Ninini hukumu ya alie acha sunna ya hay-ati?
Hataileta hiyo sunna wala hataleta sijidatus-sahwi.

Ninini hukumu ya asie weza kusimama katika sala ya faradhi?
Atasali kwa kukaa kitako, akishindwa atasali kiubavu ubavu, akishindwa atasali kichali chali, ama sala ya sunna inajuzu kwa mwenye kuweza kuisali kwa kukaa, au kusimama au kiubavu ubavu.

             wallahu allamu*******yury's law

No comments:

Post a Comment