Hukumu za uislamu ni ngapi?
Hukumu za uislamu ni tano, ambazo ni FARADHI, SUNNA, MUBAHA, HARAMU NA MAKRUHU
Faradhi ni nini?
Faradhi ni lile lililolazima kulifanya na atakapo lifanya mukallaf hupata thawabu na atakapo liwacha hupata dhambi (adhabu ).
Aina za faradhi ni ngapi?
faradhi zimegawanyika katika aina kuu mbili, ambazo ni faradhi ya lazima na faradhi ya kutosheleza.
Ni ipi faradhi ya lazima?
Faradhi ya lazima ni ile ilio lazima juu ya kila mukallaf kuifanya, kama vile kusali na kufunga.
mukallaf ni mtu alie baleghe mwenye akili timamu.
Ni ipi faradhi ya kutosheleza?
Faradhi ya kutosheleza ni ile iliyo lazima kwa mukallafina wote kuifanya lakini itakapo fanywa na mukallaf baadhi kati yao basi wote hupata thawabu.
faradhi hii sio lazima ifanywe na kila mtu ila watapo ifanya wachache basi huesabika kuwa watu wote wameitekeleza faradhi hiyo.
Sunna ni nini?
ni jambo linalo pendezeshwa kulifanya ,na mwenye kulifanya hupata thawabu na mwenye kuliwacha hapati dhambi.
Mubaha ni nini?
mubaha ni lile ambalo inajuzu kwa mtu kulifanya na kuliwacha, na mwenye kulifanya hapati thawabu na pia mwenye kuliwacha hapati dhambi.
Haramu ni nini?
Haramu ni jambo lililolazima kwa kila mukallaf kuliwacha, na mwenye kuliwacha hupata thawabu lakini pia mwenye kulifanya hupata dhambi. kama vile kunywa ulevi n.k
Makruhu ni nini?
Makruhu ni jambo linalo pendeza kuliwacha na mwenye kuliwacha hupata thawabu, lakini pia mwenye kulifanya hapati dhambi.
wallahu aalam.
No comments:
Post a Comment