SALA YA JAMAA.
Ninini hukumu ya sala ya jamaa?
Ni faradhi kifaya kwa wanaume wakaazi wa mji na uchache wake ni Imamu na maamuma.
Shuruti za sala ya jamaa ni ngapi?
shurti zake ni saba, ambazo ni;
1.maamuma anuie kumfuata imamu
2.maamuma ajue vihamo vya imamu japo kwa msaada (kwa kusikia sauti au kuona safu za mbele)
3.maamuma asiwe mbele ya imamu
4.Amkaribie Imamu ikiwa si msikitini
5.kusiwe na kizuizi baina yao
6.Maamuma amfuate imamu wake
7.Asimfuate yule ambaye itamlazimu kuja kuilipa( kuirejea) sala (baadae)
WALLAHU AALAM*******YURY'S LAW.
No comments:
Post a Comment